Mkufunzi wa Kupiga Ngoma Kutoka Cameroon
Tunamtembelea mkufunzi wa kupiga ngoma anayetokea Cameroon, anayefanya kazi katika shule ya muziki katikati ya Tokyo. Kazini nchini Japani - ni kipindi kinachomulika maisha ya watu kutoka duniani kote walioichagua Japani kuwa sehemu yao ya kazi.
Wouassi Vincent Jr. anayefanya kazi katika shule ya muziki eneo la Shibuya kama mkufunzi wa ngoma. Akiepukana na kuelezea nadharia ngumu ya muziki, anawahamasisha wanafunzi wake kuwa na hisia asili ya mahadhi, kwa mijongeo ya miili yao.
Wouassi amekuwa akisaka uundaji wa sauti mpya zinazotokana na muziki wa kitamaduni wa Kiafrika. Pia katika bendi yake, anapiga shamisen, ala ya kitamaduni ya Kijapani.