Mateusz Majewski: Mfanyakazi katika Duka la Miwani
Kazini nchini Japani - hiki ni kipindi kinachomulika maisha ya watu kutoka kote duniani walioifanya Japani kuwa kazini kwao. Safari hii, tunakutana na kijana kutoka Poland anayefanya kazi katika duka la miwani huko Kitakyushu.
Mateusz anafanya kazi katika duka la miwani. Anataka kusaidia watu kupitia kazi yake.
Mateusz na rafikiye wa dhati anayefanya naye kazi.
Mateusz anasema anataka kuwafurahisha wateja kwa kumakinikia zaidi mahitaji na upendeleo wao.