Kuzifikia Nyota! Kusaidia Kuwafunza Wanamichezo Wenye Ulemavu wa Macho nchini Laos
Kipindi cha Bega kwa Bega kinakukutanisha na wanaume na wanawake Wajapani wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea, wakishughulikia matatizo mbalimbali pamoja na wenyeji. Katika kipindi hiki utamsikia Hane Hiroyuki, anayewafundisha wanariadha wenye ulemavu katika nchi ya Laos, kusini mashariki mwa Asia. Hane, mwenye ulemavu wa mkono wa kushoto, pia alikuwa mwanamichezo mwenye ulemavu. Akiishi Laos tangu mwaka 2015, anawahangaikia wanamichezo wenye matatizo ya macho kufikia mashindano ya kimataifa. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 2, 2020.)
Hane Hiroyuki anawafunza wanariadha wenye ulemavu wa macho, akiwafundisha jinsi ya kutumia mwili wake hatua kwa hatua.
Hane Hiroyuki
Bounphet Thepthida mmoja wa wanamichezo wanaofundishwa na Hane.