Redio ya Uokoaji: Indonesia
Redio Tutura ni kituo cha redio ya kijamii kilichoanzishwa katika kisiwa cha Sulawesi kilichoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi mwaka 2018 nchini Indonesia. Kituo hicho kimelenga kutoa taarifa juu ya ujenzi mpya wa eneo hilo unaosaidiwa na shirika moja la Kijapani lisilo la kujipatia faida la FMYY. Likiwa lilianzishwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi la 1995 la Hanshin-Awaji, shirika la FMYY limekuwa likitoa huduma za redio kwa lugha mbalimbali katika mji wa Kobe magharibi mwa Japani. Kwa kutumia uzoefu kama kituo cha redio ya kijamii ya eneo lililokumbwa na janga, kituo hicho kimekuwa kikifanya kazi na Indonesia kwa zaidi ya miaka 10, nchi ambayo pia hukumbwa na majanga ya asili mara kwa mara. Kipindi hiki kinaangazia simulizi ya Wajapani na Waindonesia wanaofanya kazi ya kurejesha hali ya kawaida kwa kuendesha kituo cha redio ya kijamii. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 13, 2020.)
Redio Tutura imeanzisha matangazo kijijini Karawana huko Sulawesi.
Mkurugenzi wa FMYY Hibino Junichi (kulia) amesaidia ufunguzi wa redio ya kijamii nchini Indonesia.
Sukiman Mohtar Pratomo anayeendesha kituo cha redio huko Jawa pia alikuja kutoa ushauri.
Dewi Kurniawati, mmoja wa wafanyakazi wa mwanzo wa redio Tutura akiwafanyia mahojiano wanakijiji.