Kushinda Virusi vya Korona: Ufilipino
Virusi vya korona vimekuwa mwiba duniani kote. Vinaathiri maisha ya watu, na baadhi yao wanahangaika kupata chakula cha kila siku kwani wamekuwa wakitatizika kupata pesa tangu kabla ya janga hilo. Nchini Ufilipino, shirika lisilokuwa la serikali la Japani linaendelea na shughuli zake za kuzisaidia familia maskini, likikabiliana na hatari ya maambukizi. Tunampigia darubini Mjapani mmoja na wafanyakazi wake wanaowasilisha misaada kwa wanaoihitaji huku kukiwa na vizuizi mbalimbali. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 15, 2020.)
Mtandao ujulikanao kama International Children's Action Network, ICAN wenye makazi yake Japani unaendelea kuwasilisha misaada kwa familia za mapato ya chini huku kukiwa na korona.
Fukuta Hiroyuki ni mkuu wa tawi la ICAN nchini Ufilipino.
Mfanyakazi Mfilipino Mariditha Mondares hushiriki shughuli za ICAN huku akifanya kazi kama nesi.