Kawaguchi Kyogo na Miyamoto Karin
Leo, wageni wawili watashiriki kipindi chetu. Mgeni wa kwanza ni Kawaguchi Kyogo. Ni mwimbaji na mtunzi anayewafurahisha watu kwa sauti yake ya uimbaji inayoonekana kuwafunika kwa kumbatio lenye joto. Wimbo wake maarufu wa "Sakura" umerudiwa kuimbwa na wanamuziki nchini Japani na nje ya nchi hiyo. Mgeni wetu wa pili ni Miyamoto Karin. Ni mwanachama wa zamani wa kundi maarufu lililoitwa juice=juice. Aliachana na kundi hilo na kuwa mwanamuziki binafsi mwaka 2020. Ana sauti ya uimbaji yenye utajiri wa kuelezea hisia. Licha ya kuwa katika kundi, alianza kufanya ziara kama mwanamuziki binafsi. Tafadhali furahia mahojiano yetu ya kipekee na burudani ya muziki wao.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.