Omoinotake na Not Equal ME
Leo, wageni wawili watashiriki kipindi chetu. Wageni wa kwanza ni bendi ya Omoinotake, inayohusisha wanachama watatu ambayo imezidi kuvuta hisia za mashabiki kwa ushawishi wake lakini pia sauti za kusisimua wanapotumbuiza jukwaani na mashairi yenye hisia. Muziki wao unaochezeka na wenye hisia umezidi kupata umaarufu mkubwa nje ya Japani. Wageni wetu wa pili ni kundi maarufu lenye wanachama 12, Not Equal Me. Jina lake Not Equal Me, linaakisi matumaini ya watu kupata utofauti mpya wa kipekee.Tafadhali furahia mahojiano yetu ya kipekee na burudani ya muziki wao. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 15, 2022.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.