Tokyo Rikisha na NEMOPHILA
Leo, wageni wawili watashiriki kipindi chetu. Wageni wa kwanza ni kundi la Tokyo Rikisha linalopatikana eneo la kihistoria la Asakusa jjini Tokyo. Wanachama wanne wa kundi hili huendesha riksho za kutembeza watalii eneo la Asakusa, wakati wakiendelea na kazi zao za sanaa. Wageni wetu wa pili ni kundi la NEMOPHILA. Ni bendi ya watu watano, huwachangamsha mashabiki zao kwa matumbuizo yao ya midundo mizito. Kinyume na muziki wao, wanajulikana kwa sauti nyororo na mazungumzo ya utulivu hivyo huvutia sana kama "bendi laini kutoka kuzimu". Tafadhali furahia mahojiano yetu ya kipekee na burudani ya muziki wao.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.