Atari Kosuke na Fudanjuku
Leo, wageni wawili watashiriki kipindi chetu. Mgeni wa kwanza ni Atari Kosuke. Alianza kuimba kwenye kampuni kubwa ya muziki mwaka 2006, na sasa amefikisha miaka 16 tangu aanze kuimba. Uimbaji wake unaelezwa kuwa "unaotuliza moyo zaidi duniani." Mgeni wetu wa pili ni Fudanjuku, kundi pendwa la waimbaji saba wa kike waliovalia mavazi ya kiume. Wao daima hudhihirisha ukweli wa kauli mbiu yao, "Tutakuchangamsha." Ni waimbaji maarufu miongoni mwa wasichana wenye umri kama wao. Furahia mahojiano yetu ya kipekee nao na tumbuizo mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 3, 2022.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.