Moriguchi Hiroko and fhána
Leo, wageni wawili watashiriki kipindi chetu. Mgeni wa kwanza ni Moriguchi Hiroko. Alianza kuimba kwenye wimbo wa kutambulisha mfululizo wa katuni za runinga za anime unaojulikana kama "Mobile Suit Zeta Gundam" mwaka 1985. Hii leo, atatuimbia wimbo uliotumika kutambulisha filamu ya hivi karibuni inayoitwa Gundam, iliyozinduliwa mwezi Juni. Wageni wetu wa pili ni kundi la fhána linalojulikana kwa kuimba nyimbo nyingi za katuni za anime. Leo, wataimba wimbo kutoka katika albamu yao ya hivi karibuni iliyozinduliwa mwezi Aprili. Tafadhali furahia mahojiano yao ya kipekee na tumbuizo mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.