Morning Musume.'22
Kipindi cha leo ni maalum kwa ajili ya kundi maarufu la muziki wa pop nchini Japani linalojulikana kama - Morning Musume.'22. Kundi la Morning Musume lilianzishwa rasmi mwaka 1997 kupitia mchujo kwenye kipindi cha televisheni, na kwa sasa linatumbuiza likijulikana kama Morning Musume.'22. Huwa linabadilika, pale wanachama wanapohitimu, au kwa maneno mengine wanapoondoka kundini, na wanachama wapya kuongezwa. Na sasa linaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake. Tafadhali furahia mahojiano yao ya kipekee pamoja na tumbuizo mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.