Bendi ya Crazy Ken
Hii leo, tunakuletea tumbuizo maalum mubashara iliyofanywa na Bendi ya Crazy Ken. Mwaka huu, bendi hiyo yenye wanachama 11 inaadhimisha miaka 25 tangu kuasisiwa kwake. Mtindo wa bendi hiyo unaojumuisha tanzu mbalimbali za muziki unavutia mashabiki wa marika mbalimbali. Kiongozi wa bendi hiyo na mwimbaji, Yokoyama Ken, pia anafahamika kama mtengenezaji shupavu wa tuni, akitoa nyimbo kwa wasanii wengi maarufu nchini Japani. Tafadhali furahia mahojiano yao ya kipekee na tumbuizo zao mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.