BiS na Kaya
Leo tuna wageni wawili. Wa kwanza ni BiS, kundi la wanawake lililoundwa 2010. Kundi hilo limevutia mashabiki wengi kufuatia tumbuizo zao kali zisizokuwa za kawaida, kama vile tamasha mubashara lililodumu saa 24, au kukimbia mbio za umbali wa kilomita 200 kwa siku mbili. Mgeni wetu mwingine ni Kaya, aliyeanza tu kurekodi nyimbo zake kwenye kampuni kubwa ya muziki. Kaya ana sauti taanisi ambayo imeitwa "sauti takatifu." Ameshiriki mashindano mengi ya uimbaji na amesifiwa mno tangu alipokuwa mdogo. Furahia mahojiano nao na tumbuizo zao mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.