Kaizo Ryota na Matsuri nine.
Leo, tunawaalika wageni wawili kipindini. Wa kwanza ni Kaizo Ryota, aliyeshinda Mashindano ya Karaoke Duniani, yaliyomwezesha kuanza kurekodi nyimbo zake katika kampuni kubwa ya kurekodi muziki. Akiwa na ujuzi bora wa sauti na namna ya kujieleza, Kaizo anajulikana kama mmoja wa waimbaji vijana wenye vipaji mno kwa sasa. Mgeni wetu wa pili ni Matsuri nine, kundi la wanaume wanne kutoka Nagoya. Wakitumia mtindo wao wa sauti kali na densi, wanachama wa kundi hilo pia wanatamba katika burudani zingine, kama kumbi za sinema na filamu. Tafadhali furahia mahojiano ya kipekee na utumbuizaji wao mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 6, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.