GARNiDELiA na Suzukisuzuki
Leo, tuna wageni wawili. Wa kwanza ni kundi la GARNiDELiA. Kundi hilo lililoundwa mwaka 2010 linajumuisha mwanamume na mwanamke. Wao ni maarufu kwa kutunga nyimbo nyingi za katuni za anime. Mgeni wetu wa pili ni kundi la Suzukisuzuki. Kundi hilo linaundwa na Suzuki Tom na Suzuki Seina ambao ni ndugu. Linajihusisha zaidi na upachikaji wa video za muziki kwenye mitandao ya kijamii. Na kundi hilo limeungwa mkono na vijana wengi. Tafadhali furahia mahojiano yetu ya kipekee na tumbuizo mubashara studioni.

*Kutokana na hamiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.