Bullet Train na Nakanekana
Wageni wa leo ni Bullet Train na Nakanekana. Nakanekana ni kundi la watu wawili, mwimbaji na mpiga gitaa. Wawili hao wamepata umaarufu kwa kupachika video zao mtandaoni. Wamevutia watu kutokana na wimbo wao unaoelezea kicheshi aina za vitu vinavyotokea unaposhirikisha video kwenye tovuti, na walianza kurekodi nyimbo zao kwenye kampuni kubwa ya kurekodi muziki mwezi Julai mwaka huu. Bullet Train ni kundi la wanaume watano wanaojilinganisha na treni ya mwendokasi kwa kujipa majina ya idadi ya mabehewa kila mmoja, kuanzia mbili hadi saba. Na wanawaita mashabiki wao "behewa namba nane." Mwezi Disemba mwaka huu, kundi hilo linasherehekea mwaka wao wa kumi tangu kuundwa kwake. Tafadhali furahia mahojiano ya kipekee na utumbuizaji wao mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Disemba 4, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.