SKE48 na SCANDAL
Tuna wageni wawili studioni. Wa kwanza ni SKE48, kundi la wanawake lililoundwa mwaka 2008. Shughuli zao zikijikita mjini Nagoya, kundi hilo ni maarufu mno. Nyimbo zao nyingi zimeshika nafasi ya kwanza kwenye chati ya muziki Japani. Mgeni mwingine ni bendi ya wanawake wanne, SCANDAL. Ni maarufu si tu nchini Japani bali pia nje ya nchi hiyo, na wamekuwa wakitumbuiza kama wanamuziki solo matamashani duniani kote. Mwaka huu, wameadhimisha miaka 15 tangu kuundwa kwa bendi hiyo.Tafadhali furahia mahojiano ya kipekee na utumbuizaji wao mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.