Hikawa Kiyoshi na Takagi Reni
Leo, tuna wageni wawili. Wa kwanza ni Hikawa Kiyoshi, aliyeanza kurekodi muziki kwenye kampuni kubwa ya muziki mwaka 2000. Miaka ya hivi karibuni, uimbaji wake umevuka mipaka ya baladi za kitamaduni za enka na sasa unajumuisha tanzu zingine kama vile muziki wa pop na rock. Amekuwa akiimba kwenye vipindi maarufu vya katuni za anime. Mgeni wetu wa pili ni Takagi Reni, mwanachama wa Momoiro Clover Z, moja ya makundi pendwa maarufu zaidi nchini Japani. Hivi karibuni, amekuwa akiimba pia kama mwanamuziki solo. Kadhalika aliibua msisimko miongoni mwa mashabiki kwa kubeba mwenge wakati wa Olimpiki ya Tokyo. Tafadhali furahia mahojiano ya kipekee na utumbuizaji wao mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 16, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.