JO1 na BIGYUKI
Leo, tuna wageni wawili. Wa kwanza ni JO1, bendi ya wanaume yenye wanachama 11 waliochaguliwa wakati wa kipindi cha mchujo cha runinga. Jina la kundi hilo "JO1" linaakisi matamanio ya wanachama ya kuungana na kuwa kundi bora duniani. Mgeni wetu wa pili ni BIGYUKI, mpigaji kibodi anayefanyia shughuli zake nchini Marekani. Kipaji chake kinajumuisha tanzu mbalimbali ikiwemo miziki ya jazz, R&B na hip-hop, na ni mmoja wa wasanii marufu zaidi wa Japani kwenye tasnia ya muziki ya Marekani. Tafadhali, furahia mahojiano na tumbuizo zao za kipekee mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.