ZOC
Mgeni wa leo ni ZOC. Hili ni kundi pendwa la pop lililoundwa na mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Oomori Seiko. Shughuli za kundi hili zimejikita katika dhana ya "wapweke wasiachwe wajihisi wametengwa." Oomori Seiko ni msimamizi wa kundi hilo, lakini badala ya kujitambulisha hivyo, anasema yeye ni "mbia," yaani, ana tundu jeusi moyoni mwake sawia na wanachama wengine, na kuwa wote wanapambana na kufurahia pamoja kama kundi moja. Furahia mahojiano na utumbuizaji mbashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 10, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.