Angerme na Not Equal ME
Tuna wageni wawili katika kipindi cha leo. Wa kwanza ni Angerme, kundi la pop lenye wanachama 10. Kwa sasa, kundi hilo ni sehemu ya "Hello! Project," mradi unaoundwa na makundi matano ya pop na wakurufunzi. Wanachama wa kundi la Angerme ni maarufu kwa utumbuizaji wao mzuri. Pia wamekuwa na maonyesho ya kufana nje ya Japani. Mgeni wa pili ni Not Equal ME. Nalo ni kundi la pop linalosimamiwa na Sashihara Rino, ambaye awali alikuwa mwanachama mkuu wa kundi la pop la HKT48. Hivyo ,Not Equal ME ni kundi la wanawake 12 lililoanza muziki chini ya kampuni kubwa ya kurekodi mwaka huu. Furahia mahojiano maalum na utumbuizaji wao mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 4, 2021.)

*Kutokana na haki na vizuizi vingine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.