NMB48 na SHISHAMO
Leo, tuna makundi mawili kwenye kipindi chetu. La kwanza ni NMB48, kundi pendwa la pop lililopo Osaka, ambao ni moja ya miji mikubwa magharibi mwa Japani. Likisimamiwa na mtunzi maarufu wa nyimbo, Akimoto Yasushi, NMB48 ni kundi ndugu wa lile la AKB48. NMB48 limeibuka kuwa kundi muhimu katika tasnia ya muziki nchini Japani. Mgeni wetu wa pili ni bendi ya wanawake watatu ya muziki aina ya rock, SHISHAMO. Umri wa wanachama wote ni wa miaka ya 20. Wametumbuiza kama bendi tangu umri wao wa balehe, na SHISHAMO imekuwa bendi maarufu kutokana na mashairi na muziki wake unaovutia sana vijana. Tafadhali furahia mahojiano maalum na utumbuizaji mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 7, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.