NGT48 na Chris Hart
Leo, wageni wawili watashiriki kipindi chetu. Wa kwanza ni NGT48, kundi pendwa la pop lenye makazi yake mkoani Niigata. Moja ya maudhui ya shughuli za kundi hilo ni kufokasi kwa na kuchangia jamii ya eneo hilo. NGT48 ni kundi dada la AKB48 na lilizinduliwa na mtunzi maarufu wa nyimbo, Akimoto Yasushi. Mgeni wetu wa pili ni Chris Hart, ambaye kiasili anatoka nchini Marekani lakini anaimba nyimbo kwa Kijapani. Alianza tena kuimba kwenye tasnia ya muziki ya Japani mwaka 2020, baada ya mapumziko ya miaka miwili. Furahia mahojiano ya kipekee na tumbuizo mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.