HKT48 na MARiA
Wageni wetu leo ni wawili: wa kwanza ni HKT48, hili likiwa kundi pendwa la pop lenye makazi yake jijini Fukuoka, jiji kubwa katika eneo la Kyushu kusini mwa Japani. Ni moja ya makundi dada ya kundi la AKB48, linaloongozwa na mwanamashairi mashuhuri Akimoto Yasushi. Kundi la HKT48 limetoa nyimbo nyingi maarufu, mmoja baada ya mwingine. Mgeni wa pili ni mwimbaji solo, MARiA. Ni mwanachama wa kundi la watu wawili liitwalo GARNiDELiA lenye nyimbo nyingi maarufu za katuni za anime. Mwaka huu, MARiA pia alianza kutumbuiza kama mwimbaji solo. Furahia mahojiano maalum na walivyotumbuiza mubashara studioni.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.