Suzuki Konomi na LAST IDOL
Leo, tutakuwa na wageni wawili. Wa kwanza ni Suzuki Konomi aliyeanza kazi ya muziki akiwa kijana wa miaka ya kumi na ushei. Akiwa na umri wa miaka 24, msanii huyo mwenye kipaji amejipatia umaarufu kwa kuimba nyimbo zaidi ya 20 za kutambulisha filamu za katuni za anime. Mgeni wa pili ni LAST ADOL, kundi la muziki aina ya pop lililoundwa mwaka 2017 kupitia usaili wa kipindi kinachotayarishwa na mtunzi mashuhuri wa mashairi Akimoto Yasushi. Tafadhali burudika na mahojiano yao maalum na walivyotumbuiza mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Juni 12, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.