Namie Joshihatsu Kumiai (Shirikisho la Joshihatsu Namie)
Mgeni wetu leo ni Namie Joshihatsu Kumiai (Shirikisho la Joshihatsu Namie)! Kundi pendwa la pop linalofanyia shughuli zake mjini Namie mkoani Fukushima - mji ambao uliathiriwa mno na Tetemeko Kubwa la Ardhi lililotokea Mashariki mwa Japani mwaka 2011. Sasaki Ayaka, mmoja wa wanachama wa kundi maarufu la wanawake la Momoiro Clover Z, anahudumu kama mtayarishaji wa muziki katika kundi la Namie Joshihatsu Kumiai. Tutatambulisha shughuli zao na kusikiliza wanavyotumbuiza mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Juni 5, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.