Momoiro Clover Z na Da-iCE
Tunayaangazia makundi mawili katika kipindi hiki. Momoiro Clover Z ni moja ya makundi vinara ya wanawake nchini Japani. Kundi hilo lenye wanachama wanne limejipatia umaarufu kwa mtindo wake wa kipekee wa utumbuizaji moja kwa moja na sasa linawavutia watu wengi nchini humo. Pia tunaliangazia kundi la uimbaji na uchezaji dansi la Da-iCE, ambalo wanachama wake watano akiwemo mwimbaji anayeimba sauti nne, wakionyesa vipaji vyao vya kisanii katika nyimbo mbalimbali zinazovuma hadi nje ya mipaka ya utanzu wa muziki. Utasikia mahojiano yao maalum na walivyotumbuiza mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Mei 15, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.