Miyazawa Kazufumi, BAND-MAID, na Cho Tokimeki♡Sendenbu
Tunawaangazia wasanii watatu katika kipindi hiki. Miyazawa Kazufumi ni mmoja wa waimbaji na watunzi vinara wa nyimbo nchini Japani. Katika nyimbo zake amekuwa akichanganya aina mbalimbali za muziki aliokutana nao wakati wa ziara zake duniani. BAND-MAID ni bendi ya wanawake watano. Wakivalia mavazi ya wajakazi, wanachama wake wanajivunia ulimbwende na sauti za rock. Cho Tokimeki♡Sendenbu, ni kundi la wanawake sita. Maana ya moja kwa moja ya jina la kundi hilo ni "Idara ya umma ya furaha kubwa," likielezea tamanio la kuwasilisha tajiriba za kukonga mioyo kwa watu duniani kote. Furahia mahojiano yao maalum na walivyotumbuiza mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Mei 8, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.