Sakamoto Fuyumi, Morning Musume。'20, na kundi la Bullet Train
Kwenye kipindi hiki, tunawaangazia wasanii watatu. Sakamoto Fuyumi ni mmoja wa waimbaji vinara wa baladi ya kitamaduni ya enka nchini Japani. Kipaji chake ni zaidi ya kuimba nyimbo hizo -- alikuwa na nyimbo zilizovuma kutoka tanzu mbalimbali za muziki. Morning Musume。'20 ni kundi linalojivunia umaarufu mkubwa nchini Japani na kwingineko. Bullet Train ni kundi la kipekee la wanaume watano. Kila mwanakundi amepewa namba ya behewa kati ya mbili na saba. Utasikia mahojiano yao maalum na walivyotumbuiza studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 16, 2021.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.