Miyano Mamoru na JO1
Katika kipindi hiki, tutamwangazia msanii mwanamume na kundi la wanaume. Tunaanza naye Miyano Mamoru, muigizaji maarufu wa sauti anayefahamika kwa kuigiza kama mhusika mkuu katika mojawapo wa vipindi vya "Mobile Suit Gundam", mfululizo wa runinga wa katuni za anime ambao ni maarufu siyo tu nchini Japani bali pia kote duniani. Pia anajishughulisha sana na uimbaji, na ana uwezo wa kujaza mashabiki katika viwanja na maeneo mengine makubwa. Wa pili kuangaziwa ni JO1, kundi linalojumuisha wanaume 11. Wanachama wote wapo katika umri wa chini ya miaka 20 na miaka ya 20, na waliwashinda wapinzani wao katika kipindi cha usaili wa kipindhi cha runinga. Mara ya kwanza kwa kundi la JO1 kutoa rekodi yake ilikuwa mwezi Machi, 2020. Nyimbo zote zilizozinduliwa na kundi hilo zimewekwa kwenye chati. Furahia mahojiano yao maalum na utumbuizaji mubashara studioni!

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakipatikani utakavyo.