Moriguchi Hiroko na SILENT SIREN
Kipindi hiki kinawaangazia Moriguchi Hiroko na SILENT SIREN. Moriguchi Hiroko alianza uimbaji mwaka 1985, akiimba wimbo ashiria wa "Mobile Suit Zeta Gundam," ambao ni mfululizo wa katuni za anime unaopendwa sana Japani. Ni mwimbaji mwenye kipaji asiyejifungia kwenye nyimbo aina ya pop pekee. Pia anajaribu kufanya matamasha ya muziki wa jazz. SILENT SIREN ni bendi ya muziki ya wanawake wanne. Wote wameangaziwa kama wanamitindo kwenye majarida. Kwa hivyo, wamejizolea umaarufu kwa mionekano yao ya kupendeza na kipaji cha muziki. Tunakuletea mahojiano yao maalumu na nyimbo walizoimba studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 10, 2020.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakiwezi kupatikana kadiri utakavyo.