Marty Friedman, Kitagawa Rio (Morning Musume.'20), na Funaki Musubu (Angerme)
Tutaangazia nyimbo za J-pop zilizoimbwa upya na wasanii watatu. Wa kwanza ni Marty Friedman. Ni mpiga gita mwenye asili ya Marekani. Hata hivyo, baada ya kuupenda mno muziki wa Japani, alihamia nchini humo na amekuwa akitumbuiza tangu wakati huo. Mgeni wetu wa pili ni Kitagawa Rio, ambaye ni mwanachama wa kundi pendwa la pop kwa jina Morning Musume.'20. Kitagawa Rio ini mwanachama mpya aliyejiunga na kundi hilo mwaka jana. Na mgeni wetu wa tatu ni Funaki Musubu, ambaye ni mwanachama wa kundi pendwa la pop la Angerme. Ameshiriki maonyesho mengi nje ya Japani na pia ana mashabiki wengi duniani kote. Utasikia mahojiano yao maalum na walivyotumbuiza studioni.

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.