Mizuki Nana, Hirai Miyo (BEYOOOOONDS), na Nojima Kano (SKE48)
Leo tunawaangazia Mizuki Nana, Hirai Miyo, na Nojima Kano. Mizuki Nana ni mmoja wa waigizaji maarufu wa sauti nchini Japani, aliyeigiza sauti za wahusika wa katuni za anime katika maonyesho mengi maarufu. Pia amejipambanua kama mwimbaji, akivuta nadhari ya hadhira kwa utumbuizaji wake mzuri kwenye matamasha ya moja kwa moja. Hirai Miyo ni mwanachama wa kundi pendwa la pop la Beyooooonds. Ataimba upya wimbo maarufu wa J-pop. Nojima Kano, kutoka kundi pendwa la pop la SKE48, ataimba upya wimbo ashiria wa filamu maarufu kimataifa ya katuni za anime. Pia utasikia mahojiano na walivyotumbuiza studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 7, 2020.)

*Kutokana na hakimiliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakipatikani kadiri utakavyo.