WAGAKKIBAND na BOYS AND MEN
Wakati huu tutawaangazia WAGAKKIBAND na BOYS AND MEN. WAGAKKIBAND inajizolea umaarufu kwa mtindo wake mpya na wa kipekee, unaojumuisha ala za kitamaduni za Kijapani katika muziki wa rock. Bendi hiyo yenye wanamuziki wenye vipaji imekuwa na matamasha ya kufana ndani na nje ya Japani. BOYS AND MEN ni kundi la muziki lenye wanaume tisa wanaoweza kuimba, kucheza dansi na kutumbuiza jukwaani au katika maigizo na uimbaji. Kundi hilo limevutia hadhira zaidi ya 20,000 kwenye tamasha. Tunakuletea mahojiano maalum na makundi hayo pamoja na utumbuizaji wao moja kwa moja kutoka studioni.

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakipatikani utakavyo.