Frederic na Tsubaki Factory
Wakati huu tunaangazia Frederic na Tsubaki Factory. Frederic ni bendi ya wanaume 4 iliyobuniwa na kaka pacha Mihara Kenji and Mihara Koji. Ilianza kurekodi muziki kwenye kampuni kubwa ya kurekodi muziki mwaka 2014. Ni bendi iliyojizolea umaarufu kutokana na tumbuizo zake mubashara, mahadhi yake yenye mitindo mbalimbali ya muziki na mashairi yenye ucheshi kiasi. Nalo kundi la Tsubaki Factory linajumuisha wasichana 9 na lilianza kurekodi muziki wake kwenye kampuni kubwa ya kurekodi muziki mwaka 2017. Kundi hilo ni sehemu ya "Hello! Project," inayoundwa na makundi pendwa ya pop 5 na wanagenzi. "Tsubaki" ni neno la Kijapani la "camellia" ambalo ni ua lililoenziwa na Wajapani tangu enzi za kale. Tunakuletea mahojiano maalum na tumbuizo mubashara studioni.(Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 17, 2020.)

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakipatikani utakavyo.