ANGERME, Miyamoto Karin, na Kiyono Momohime
Kipindi cha leo kinaangazia ANGERME, Miyamoto Karin na Kiyono Momohime. Kundi na wasanii wawili ni kutoka kundi la wasichana la "Hello! Project," lililo na makundi matano na wakurufunzi. "S/mileage" lilibadilishwa jina mwaka 2014 na kuitwa ANGERME, ni kundi pendwa linalofanya matamasha ya kufana nje ya nchi. Miyamoto Karin ni mwanachama wa kundi la Juice=Juice ambaye pia amekuwa akifanya shughuli zake kama msanii solo. Kiyono Momohime ni mwanachama wa kundi jipya kabisa la BEYOOOOONDS la mradi wa Hello! Project. Tunakuletea mahojiano na nyimbo walizoziimba wakiwa studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 12, 2020.)

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakitopatikana utakavyo.