AK-69 & Coba
Katika kipindi hiki, tutakuwa na AK-69 na Coba. AK-69 ni mwanamuziki wa kufoka aliyesifiwa sana nchini Marekani kulikochipukia muziki huo. Amejizolea mashabiki miongoni mwa wanamichezo wa kulipwa pia. Coba ni mpiga kadioni anayecheza muziki wa pop kwa kutumia ala hiyo ambayo kwa kawaida uhusishwa na muziki dhati na anatumbuiza duniani kote. Furahia mahojiano ya wasanii hao wawili na wanavyotumbuiza moja kwa moja kutoka studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa 08 Agosti 2020.)

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakitopatikana utakavyo.