Sasaki Ayaka na Kundi la Bullet Train
Kipindi hiki kinamwangazia Sasaki Ayaka na kundi la Bullet Train. Sasaki Ayaka ni mwanachama wa kundi la Momoiro Clover Z, kundi pendwa maarufu la wanawake. Ametoa albamu yake ya kwanza akiwa solo mwezi Julai mwaka huu. Kundi pendwa la wanaume la Bullet Train linavuma nchini Japani.  Linajizolea umaarufu kwa mtindo wao mpya na wa kipekee, huku wakibadili mchezaji dansi kinara katika kila ya nyimbo zao. Tunakuletea mahojiano yao adimu pamoja na tumbuizo mubashara studioni. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 15, 2020.)

*Kutokana na hakimiliki na masharti mengine, kipindi hiki hakitopatikana utakavyo.