Ayaka Hirahara & Morisaki Win
Ayaka Hirahara na Morisaki Win wanashiriki. Ayaka Hirahara alianza rasmi muziki kwa wimbo wake wa "Jupiter," ambao ameambatanisha mashairi ya Kijapani kwenye muziki wa bora wa Gustav Holst. Ulikuwa wimbo uliovuma sana. Morisaki Win alizaliwa nchini Myanmar na kuhamia Japani alipokuwa mwanafunzi wa shule ya msingi. Mwaka huu ametokea kwenye tamthiliya ya runinga ya Myanmar. Tunakuletea mahojiano na wasanii hao wawili na nyimbo walizoimba wakiwa studio. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 18, 2020.)

*Kutokana na haki miliki na makatazo mengine, kipindi hiki hakitopatikana kwenye on demand