Pigmenti Zing'aazo Gizani
Simulizi kuhusu bidhaa maarufu na uvumbuzi kutoka Japani. Hiki ni kipindi cha Uvumbuzi Kutoka Japani. Wakati huu, tunaangazia pigmenti zinazong'aa gizani, zinazosharabu mwanga ili kung'aa gizani. Aina ya pigmenti hizi ambazo hazina dutu za mionzi hatari zilivumbuliwa nchini Japani mwaka 1993. Na sasa zinatumika duniani kote katika bidhaa kama saa na alama za dharura. Tunafahamu simulizi zilizofichama katika utengenezaji wa pigmenti hizo ikiwa pamoja na namna zilivyoanza kutengenezwa na kampuni iliyokuwa hatarini kufungwa. (Kipindi hiki kilitangazwa Mei 5, 2021.)
Pigmenti ziking'aa baada ya kusharabu mwanga.
Alama ya dharura iliyopakwa pigmenti.
Nemoto Ikuyoshi, mwenyekiti na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni iliyovumbua pigmenti.
Aoki Yasumitsu, aliyesimamia uendelezaji wa pigmenti.