Cherehani Zinazokata Uzi Zenyewe
Simulizi zinazoelezea bayana  bidhaa maarufu na uvumbuzi kutoka Japani: hiki ni kipindi cha Uvumbuzi kutoka Japani. Wakati huu, tunaiangazia bidhaa inayotumika na kupendwa katika viwanda vya nguo kote duniani: cherehani zinazokata uzi zenyewe. Kanyaga tu pedali kwa mguu, na nyuzi zilizoambatanishwa kwa vipande vya nguo zinakatwa moja kwa moja. Kutoka nembo za hali ya juu hadi mitindo ya kisasa, cherehani hizi zinatumiwa na washonaji kote duniani. Wakati huu, tunazamia katika simulizi isiyojulikana na wengi juu ya uvumbuzi wa cherehani hizo.
Cherehani ya kwanza inayokata uzi yenyewe, iliyotengenezwa mwaka 1969.
Shinomiya Hiroaki, mwanachama wa timu iliyovumbua cherehani hiyo.
Aina mpya ya sasa ya cherehani hiyo.