Kamera Ndogo za Video
Simulizi kuhusu bidhaa maarufu na uvumbuzi kutoka Japani: hiki ni kipindi cha Uvumbuzi kutoka Japani. Wakati huu, tunaziangazia kamera ndogo za video zinazotumika duniani kote. Mwaka 1989, kampuni moja ya Japani ilitengeneza kamera ndogo na nyepesi zaidi duniani, iliyokuwa na urefu wa pasipoti ya Japani. Iliwasaidia watu kunasa kumbukumbu muhimu, kama ukuaji wa watoto wao na matukio mengine muhimu. Tunaangazia simulizi isiyofahamika ya uvumbuzi wa kamera hizo. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 4, 2020.)
Ikizinduliwa mwaka 1989, hii ilikuwa kamera ya video iliyo nyepesi zaidi wakati huo.
Kamera hiyo ilikuwa na urefu wa pasipoti ya Japani.
Mmoja wa wanatimu ya uendelezaji, Nakagawa Katsuya.
Kamera ndogo za video zinaendelea kuwa ndogo zaidi na zaidi.