Mashine ya Kuoka Mkate Nyumbani
Simulizi kuhusu bidhaa na ubunifu kutoka Japani: hiki ni kipindi cha Uvumbuzi kutoka Japani. Wakati huu, tunaangazia mashine ya kuoka mkate nyumbani. Mashine hizi ambazo kwanza zilitengenezwa nchini Japani mwaka 1987, zinakuwezesha kuoka mkate nyumbani kwa kuweka tu viambato na kubonyeza kitufe. Ni bidhaa pendwa duniani, huku zaidi ya bidhaa milioni 10 zikiwa zimeuzwa katika nchi na maeneo 26. Tunakuletea simulizi isiyofahamika kuhusu miaka mitatu ya kazi ngumu ya kutengeneza mashine hiyo. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 2, 2020.)
Modeli ya sasa ya mashine za kutengeneza mkate nyumbani
Modeli ya kwanza ya mashine ya kutengeneza mkate nyumbani
Mkate uliookwa kwa modeli ya kwanza ya mashine ya kutengeneza mkate
Watanabe Koyomi, anayefanya kazi katika kampuni iliyovumbua mashine hizo