Karatasi za Jeli za Kupooza Joto
Simulizi kuhusu bidhaa maarufu na uvumbuzi kutoka Japani: Hiki ni kipindi cha uvumbuzi kutoka Japani. Wakati tunakutambulisha, karatasi za jeli za kupooza joto, ambazo zinaweza kuwekwa kwenye paji la uso kwa ajili ya kushusha homa. Karatasi hizi zimevumbuliwa Japani mwaka 1994, na zilihamasishwa na chakula fulani cha baa! Karatasi hizo sasa zinauzwa kwenye nchi na maeneo 20, na karibu karatasi milioni 400 zinauzwa kwa mwaka. Ungana nasi kugundua simulizi kuhusu karatasi hizo za Japani.
(Kipindi hiki kilitangazwa Julai 8, 2020.)
Karatasi za jeli za kupooza joto
Miyanishi Kazuhito, mmoja wa wanatimu ya uvumbuzi
Bidhaa hizo kwenye maeneo mbalimbali duniani
Mtoto akitumia karatasi ya jeli ya kupooza joto