Simulizi ya leo inaelezea kisiwa kidogo cha Watakano ambacho kipo tu nje ya pwani ya Pasifiki ya mji wa Shima katika mkoa wa Mie, katikati mwa Japani. Kilipata kufahamika kwa kuwa na baa na klabu za usiku kabla ya uchumi wake kudhoofika. Kijana mmoja alifika kisiwani hapo baada ya kujijenga tena kimaisha akiwa katika jiji kubwa. Kazi yake ni kusaidia kufufua kisiwa hicho kama sehemu ya juhudi za kuhuisha uchumi za watu wa kisiwa hicho. Kijana huyo na wakazi wa kisiwa hicho, wote wanajaribu kurejesha maisha yao katika msitari. (Kipindi hiki kilitangazwa Februari 28, 2023.)
Wakazi wa kisiwa hicho waliuomba mji kuwapatia mtu wa kusaidia kuhuisha uchumi wa jamii yao. Maafisa wa mji waliamua kumtuma Toge Hiroyuki.
Kisiwa cha Watakano kipo umbali wa takriban dakika tatu kwa kutumia usafiri wa boti kutoka sehemu kuu za mji wa Shima, mkoani Mie.
Kisiwa hicho kilikuwa kivutio cha watalii. Klabu za usiku zilianza kuondoshwa kisiwani humo karibu mwaka wa 1990, na jamii ya eneo hilo kushuka kiuchumi.
Takriban watu 170 wanaishi hapa -- karibu nusu yao ni wazee.