Maua ya Dansi ya Okinawa Mbali na Nyumbani
Kata ya Taisho jijini Osaka ina idadi ya watu zaidi ya 60,000. Inakadiriwa kwamba robo ya wakazi wa eneo hilo ama walihamia hapa kutoka mkoani Okinawa au ni ndugu wa waliohamia. Sio jambo la kushangaza, eneo hilo linaitwa "Okinawa Ndogo." Watu wa hapa wamehifadhi dansi ya kitamaduni ya Okinawa iitwayo "Eisa." Eisa hutumbuizwa mkoani Okinawa wakati wa Bon, kipindi ambacho roho za mababu huaminika kurejea kutembelea eneo hilo. Watu hucheza dansi hiyo kwa ajili ya mababu zao kama njia ya kuwatukuza. Wakipiga ngoma kubwa na ndogo, washiriki hujipanga katika mistari ili kupita mitaa ya jamii yao. Tumeangazia kundi la watoto la Eisa ambalo limekuwa likifanya mazoezi kwa ajili ya onyesho lijalo, la kwanza kufanyika katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 31, 2023.)
Kundi la watoto limekutana katika ukumbi wa kufanyia mazoezi wa shule ya msingi katika eneo hilo. Ni kundi la dansi ya Eisa la watoto wa Okinawa lenye wanachama 30.
Takriban nusu ya wanachama wake wana asili ya Okinawa.
Kakihana Yoshimori amekuwa akifundisha dansi ya Eisa kwa watoto kwa takriban miaka 40.