Tumetembelea kundi la "wadaiko" wapigaji wa ngoma wa Kijapani waliopo mkoani Osaka. Kundi hilo linaundwa na akinamama wenye watoto wanaosumbuliwa na magonjwa magumu kupona. Kundi hilo liko katika maandalizi ya tumbuizo lao la kwanza katika kipindi cha miaka mitatu na nusu baada ya mapumziko marefu kutokana na janga la virusi vya korona. Tunakuletea habari za ndani za kundi hilo. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 3, 2023.)
Mtoto wa kwanza wa kiume wa mmoja wa wanachama wa kundi hilo, Morimoto Junko mwenye umri wa miaka 14, Riku, ana ulemavu mkubwa. Anahitaji kusaidiwa kwa kila kitu ikiwemo kutembea hadi kuvalishwa nguo.
Mmoja wa wanachama wengine ni Nomura Yuka. Miezi sita baada ya Yuko kujiunga na kundi hilo katika msimu wa chipukizi, mwanaye wa kike Waka alifariki.