Kuokoa Maisha katika Kisiwa Kilichotengwa
Baada ya miongo mitatu akiwa bara, daktari kijana anarejea katika eneo alilozaliwa kwenye kisiwa kilichopo kaskazini ya mbali mwa Japani. Anaacha kazi yake ya udaktari wa upasuaji katika mstari wa mbele wa sekta ya dawa, ili kuchukua majukumu ya kliniki ya eneo analotoka ambayo baba yake aliisimamia kwa miaka 36. Katika jukumu hilo, anahusika siyo tu katika eneo la afya pekee bali pia maisha ya kila siku ya wagonjwa wake. Tunamfuatilia daktari huyu aliyejitolea katika mizunguko ya kila siku katika eneo hilo akiwasaidia wagonjwa kupata huduma bora inayowezekana na pia kuishi maisha kwa ukamilifu. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 1, 2022.)
Kama daktari wa kisiwa, Masuda Akio huwatembelea wagonjwa wake nyumbani na kuwapa uangalizi binafsi.
Rebun ni kisiwa kilicho kaskazini ya mbali mwa Japani chenye wakazi 2,300.
Masuda aliamua kurejea kisiwani hapo kwa sababu baba yake, aliyekuwa akisimamia kliniki kwa miaka mingi amekaribia kustaafu.