Shangazi wa Besiboli
Leo tumeitembelea timu inayoshiriki Ligi ya Watoto ya mchezo wa Besiboli jijini Osaka. Inajivunia idadi kubwa ya wachezaji 140 na ni moja ya timu zenye nguvu kwenye ligi hiyo nchini Japani. Mwanzilishi wa timu hiyo, Tanahara Yasuko, bado anashiriki vilivyo kwenye mchezo huo akiwa katika umri wa miaka ya 80. Amekuwa akifundisha kwa miaka 50. Maadili ya kijamii yamebadilika, hususani kuhusu makuzi ya watoto. Yasuko kila mara hutilia shaka mbinu zake lakini falsafa yake haibadiliki. Shangazi wa Besiboli na wanawe. Tumewaangalia watoto hawa wanavyocheza na kukua. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 4, 2022.)
Tanahara Yasuko, Shangazi wa besiboli (kushoto).