Kutafuta Uhuru kwenye Bwawa la Kuogelea
Tumetembelea shule ya kuogelea iliyopo mjini Hamamatsu mkoani Shizuoka, katikati mwa Japani. Shule hii ilifunguliwa miaka 30 iliyopita kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Suzuki Takayuki, aliyeshinda medali tano kwenye Paralimpiki ya Tokyo 2021, pia ni mmoja wa wanafunzi aliyehitimu hapo. Tunaangazia namna shule hiyo ilivyoweza kupanua upeo wa wanafunzi wengi wenye ulemavu. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 30, 2022.)
Shule hiyo, iitwayo Penguins Village Swimming School, huendesha mafunzo kila juma katika mabwawa manne ya umma yaliyopo mjini humo. Kocha Ito Yuko alianza kutoa mafunzo hayo miaka 30 iliyopita.
Suzuki Takayuki, aliyeshinda medali tano kwenye Paralimpiki ya Tokyo 2021, pia ni mmoja wa wanafunzi aliyehitimu hapo.